Thursday, July 31, 2014


Ni tukio la aina yake lililojaa kila aina ya ubaguzi wa rangi,ni wiki iliyopita kijana aliyekuwa akifanya kazi ktk mgodi wa Bulyanhulu wa Barrick,amefukuzwa kazi baada ya kuonyesha hisia zake kwa binti wa kihindi raia wa South Africa,ambaye naye ni expart wa mgodi ule.

Walipeana namba za simu,kijana wa watu akatupa ndoana kujaribu bahati yake,mambo yakamgeuka,binti mbaguzi kashtaki kwa makaburu wa mgodini,kesi ikaitishwa,hukumu ikatoka kuwa kavunja sheria kwa kumnyanyasa kimapenzi,kazi ikaisha.
Ajabu ni kuwa weusi huwa wanatongozana lakini hakuna kesi,wala kufukuzwa kazi lakini baada ya mweusi kumtongoza mweupe,kibao kikageuka kuwa ni sexual harassment.
Tukio hili limepandisha hasira watu,kwanini mtu abaguliwe ndani ya ardhi yake na wageni tu tena wenye njaa waliokuja kujistiri kwetu?
Nimeongea kwenye simu na huyu kijana,wiki ijayo naelekea Bulyanhulu ili kuonana naye nimshawishi aipeleke mahakamani kampuni hii.

0 comments:

Post a Comment