Wednesday, July 30, 2014

download
Na Mahmoud Ahmad ARUSHA
 VIONGOZI  wa ngazi za juu Serikalini wametakiwa kushirikiana na waasisi wa vyama hasa mabalozi wa vitongoji kutokana na wao kuwatambua wananchi wao kwa kiwango kikubwa hivyo kuweza kukuza chama  na kupunguza uhalifu.Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha  wakati wa ziara ya chama cha mapinduzi ccm kutembelea wilaya na kata kwa  wajumbe makatibu wenyeviti waasisi wa vyama pamoja na mabalozi kwa lengo la kujadili muongozo wa chama na changamoto zinazo kumba baadhi ya kata.Bwana Nangole alianza ziara hiyo katika Kata ya Sokoni One ambapo aligundua kero mbalimbali ikiwemo ukosefu wa maji ,Zahanati pamoja na kutokumaliziwa kwa kituo cha polisi ambacho ujenzi wake ulianza kwa muda  mrefu.

Pia katika kata ya Terati Mh.Nangole aliombwa na diwani wa kata hiyo  kuwasaidia kushughulikia  eneo kwa ajili ya kujenga Shule ya Msingi kutokana na wanafunzi wa eneohilo la Terati kutembea umbali mrefu kwenda kataika shule za jirani jambao ambalo linsababisha ajali za mara kwa mara hasa kwa watoto wadodo 
Aidha aliwataka Viongozi wa kata hiyo kutowatenga mabalozi Kwani wao ndio msaada mkubwa hasa kipindi cha uchaguzi hivyo waendelee kuwajali na kuwatumia kwani watajua utofauti mbalimbali ya chama hicho na kujua namna ya kutatua kupitia kwao
Kwa pande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha Dr Wilfed Soilel alisema kuwa chama cha mapinduzi ni chama kinachowajali wananchi wake kwa nyanja mbalimbali bila ubaguzi hivyo wamefanya ziara hiyo ili kuyabaini matatizo yanayowakabili wananchi na kuyafanyia utekelezaji kabla ya uchaguzi mkuu.
Aidha Dr soilel alisema kuwa CCMni chama tawala hivyo hakina budi kusimamia nakutetea wananchi wake bila kujali chama au uondozi wa mtu katika Kata aliyopo hivyo wataakikisha wanawachukulia hatua vuongozi ambao wanaenda kinyume na utaratibu wa haki za binaadamu kwa kutowajengea muundombinu rafiki katika maeneo yao
Naye Katibu wa wilaya mkoa wa Arusha Bwana Elisante Kimaro  alisema kuwa watahakikisha kero zote walizopata katika hizo  wanazifanyia utekelezaji kwa kufuata ilani ya chama cha mapinduzi CCM bila ubaguzi wowote.
Vilevile Mwasisi wa chama cha mapinduzi ccm kata ya Terati Mwinjilist Benjamini Mollel alisema kuwa wastaafu wa chama wanapomaliza uongozi wao wasisahaulike kwani ndio shina katika chama na watendaji wakubwa  hivyo wanatakiwa wapewe ushirikiano na kupewa nafasi ya kutoa ushauri kwani mawazo yao bado yanahitajika katika kukisaidia chama.
Hata hivyo Ziara na mikutano hiyo inalengo la kukiimarisha chama na kujua changamoto zinazokikabili chama cha mapinduzi wakati  huu wakuelekea kwenye chaguzi za Serikali ya mitaa pamoja na uchaguzi Mkuu

0 comments:

Post a Comment