Kesi hizo za udhalilishaji ni kutokana na kusambaza picha za utupu, vitisho, ununuzi/uuzaji wa binadamu na udanganyifu zimefunguliwa kwenye Mahakama moja jijini Yaounde, Cameroon ambapo aliezifungua ni aliyekuwa mchumba wake wa zamani Hélène Nathalie Koah.
Eto’o amekanusha kuhusika na hilo na katika kujibu mapigo mchezaji huyo anayeongoza kwa kutwaa tuzo nyingi za uchezaji bora barani Afrika, amefungua kesi ya matumizi mabaya ya fedha($410,755) alizompa Ms Koah kwa ajili ya kufungua taasisi ya kusaidia jamii wakati walipokuwa wapenzi.
0 comments:
Post a Comment