Aliyekuwa mke wa George Otieno, 'Tyson', Beatrice Shayo
Jamani! Katika
hali ya kushangaza, mastaa wa filamu Bongo wamesusia kumbukumbu ya siku
40 ya aliyekuwa muongozaji maarufu wa filamu nchini, George Otieno
‘Tyson’ aliyefariki dunia kwa ajali Mei 31, mwaka huu.hughuli
ya 40 ya Tyson ilifanyika Alhamisi iliyopita nyumbani kwa aliyekuwa
mkewe, Beatrice Shayo maeneo ya Sinza-Mapambano, Dar ambapo mastaa
mbalimbali walialikwa lakini hakuonekana hata mmoja hali iliyosababisha
chakula na futari iliyokuwa imeandaliwa kubaki huku wasanii wa vikundi
waliohudhuria wakirudia mara mbilimbili.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba
Akizungumza
na gazeti hili, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon
Mwakifwamba aliyekuwa kwenye shughuli hiyo alisema anashangaa mastaa wa
filamu kukacha ishu hiyo kwani alimpa taarifa Mwenyekiti wa Bongo Movie
Unity, Steven Mengere ‘Nyerere’ kwamba awaambie wahudhurie.
“Nimewaalika
wasanii wote lakini hakuna aliyekuja hata mmoja, ukweli wasanii hatuna
ushirikiano kwani Tyson ndiye mwanamapinduzi aliyeigeuza sanaa kutoka
kwenye kuuza sura hadi kuwa biashara hivyo walipaswa kumpa heshima
yake,” alisema Mwakifwamba.

0 comments:
Post a Comment