Uchovu kwa madereva wanaotumia vyombo vya moto kama Magari hupelekea dereva kusababisha ajali akiwa barabarani. Kundi la makampuni yanayo jihusisha na masuala ya kiteknolojia waliamua kuunganisha nguvu na Chuo kikuu cha Manchester huko Uingereza na idara ya masuala ya biomechanics ya huko Hispania na kua na kile walicho kiita kisayansi luwa ni "HI-TECH SEATBELT"
Mikanda hii ambayo ni ya kwenye magari itakuwa inawekwa kitu ambacho kinajulikana kama "sensor" ambacho kitakuwa kikisoma na kudhibiti mapigo ya moyo ya dereva huku kava la siti ya dereva likiwa linapima kiwango cha upumuaji cha dereva pia kompyuta ndogo ambayo itakuwepo kwenye dashibodi ya gari itakuwa ikichambua taarifa na kuondoa moja kwa moja makelele yanayoletwa na gari na kufahamu kama dereva atakuwa anasinzia au la.
Mradi huu unajulikana kwa jina la "Heart And Respiration In-Car Embedded Non-intrusive Sensors" au "HEARKEN" na umedhaminiwa na Umoja wa Ulaya.
Pia teknolojia hii imeshafanyiwa majaribio katika barabara zilizofungwa lakini wanateknolojia hiyo wamesema hivi karibuni wataanza kuifanyia majaribio teknolojia hiyo sehemu zingine.

0 comments:
Post a Comment