Tuesday, August 19, 2014

Wakazi wa Dar es Salaam ambao ni walemavu wa ngozi (albino) wakionesha hisia zao nje ya Kituo cha Polisi Buguruni, Dar es Salaam baada ya mtuhumiwa wa kutishia mauaji ya mwenzao aliyefikishwa kituoni hapo jana kudaiwa kuachiwa kwa dhamana jambo ambalo walilipinga. (Picha na Fadhili Akida).

Wakazi wa Dar es Salaam ambao ni walemavu wa ngozi (albino) wakionesha hisia zao nje ya Kituo cha Polisi Buguruni, Dar es Salaam baada ya mtuhumiwa wa kutishia mauaji ya mwenzao aliyefikishwa kituoni hapo jana kudaiwa kuachiwa kwa dhamana jambo ambalo walilipinga.Watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), jana walizua tafrani Kituo cha Polisi Buguruni, wakipinga dhamana kwa mshtakiwa, Ombeni Swai (34), mkazi wa Tabata Matumbi anayekabiliwa na kesi ya kutoa vitisho vya kumuua mwenzao.
Tafrani hiyo ilianzia katika Mahakama ya Mwanzo Buguruni baada ya mshtakiwa huyo kusomewa mashtaka na Karani wa Mahakama, Edwin Wandanda na kisha Hakimu Mfawidhi, Benjamin Mwakasonda aliyekuwa akiisikiliza kusema dhamana ya mshtakiwa iko wazi.
Polisi wa Kituo cha Bungurini wakiwa na silaha zinazodaiwa kutumiwa kuwatawanya watu wenye ulemavu wa ngozi kitioni hapo wakati wakizuia gari ilikuwa imebeba mtu anayetuhumiwa kumuua Albino baada ya kufunguliwa mashitika katika Mahakama ya Mwanzo Buguruni.PICHA ZAIDI>>

0 comments:

Post a Comment