Mshambuliaji wa zamani wa Manchester City Mario Balotelli anatarajiwa
kukamilisha uhamisho wake uliogharimu kiasi cha pauni milioni 16
kuelekea Anfield akitokea AC Milan hii leo.
Balotelli atalipwa kitita cha pauni 120,000 kwa wiki liverpool
Winga wa zamani wa Everton Kevin Kilbane ana matumaini kuwa Balotelli
ataleta mabadiliko ya haraka sana ambayo Liverpool inahitaji, chini ya
kocha Brendan Rodgers
Hata hivyo taratibu za kuangusha wino hazitafanyika kwa haraka ili
kumuwezesha kukabiliana na waajiri wake wa zamani, ambapo hii leo
patachimbika katika uwanja wa Etihad Liverpool itakapovaana na
Manchester city.
Baloteli ameichezea kwa mafanikio Manchester
City kwa miaka miwili na nusu hata hivyo amekuwa akikemewa mara kadhaa
kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu.
Pamoja na hayo Liverpool inategemea mazuri
kutoka kwake huku Rodgers akitarajiwa kumuweka Balotelli kwenye mstari
wakati wote atakapoitumikia Liverpoo
.
0 comments:
Post a Comment