Tuesday, August 5, 2014

Tunaomba sana msaada wako wa kututangazia kwenye blog yako ya jamii na wananchi kupotelewa na mtoto wetu Faith Charles Ruhembe. Amepotea tangu 31.07.2014 saa saba mchana, eneo la makumbusho usalama. Ni binti wa miaka tisa (9) na anasoma shule ya msingi Martin Luther Dodoma.

Usalama ni kwa shangazi yake Catherine Ruhembe, ambaye ni shemeji yangu na dada wa mke wangu Carolyne Ruhembe. Tumeshatoa taarifa vituo vya polisi na TV pia.

Pamoja na ujumbe huu, naambatanisha picha yake  kwa ufafanusi zaidi. Kwenye picha ni huyo binti. Ikiwa ufafanuzi zaidi ya huu utahitajika, basi napatikana kwa number hii 0715 119893.

0 comments:

Post a Comment