Wednesday, August 6, 2014

Baada ya kupata Tuzo mbili za Afrimma Diamond Plutnumz amedhamiria kufanya show ya kuushtua ulimwengu jijini London, Uingereza.

Show hiyo inayotarajiwa kufanyika mnamo tarehe 14/09/2014, Diamond atashirikiana na wakali kutoka Nigeria akiwemo mzee wa Skelewu Davido na mrembo wa Eminado Tiwa Savage na wakali wengine kibao watatikisa jiji la London katika ukumbi wa Academy.


Hata hivyo Diamond amefunguka katika ukurasa wake wa Instagram kuwa "Nimebahatika kufanya show nyingi sana Uingereza lakini kiukweli Show hii nimepania sana, nia na lengo langu ni kubwa ni kuonesha ulimwengu ni kwa kiasi gani Afrika Mashariki tumejaliwa uwezo kwenye sanaa ya muziki".

0 comments:

Post a Comment