Posted by Williammalecela.com on Friday, August 29, 2014
Florah Mbasha: Mimba niliyonayo ni ya Mume wangu sio ya Gwajima
SIKU
chache baada ya minon'gono kuibuka chini chini kuwa mwimbaji maarufu wa
nyimbo za Injili nchini Tanzania ambaye pia ni Mke wa Emmanuel Mbasha,
kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na Mchungaji wa Kanisa la kanisa la
Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima ameibuka na kukanusha madai hayo.
Akijibu maswali ya mashabiki wake wakati akichati moja kwa moja 'live' kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachofanyika kila siku ya Jumatano kuanzia saa Sita kamili amesema kuwa
hawezi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu ambaye ni ndugu yake hivyo
Mchungaji Gwajima ni mjomba wake na si mpenzi wake kama ambavyo watu
wamekuwa wakizungumzia suala hilo kwa kile alichodai ni baadhi ya watu
wanaotaka kumchafulia jina na hadhi aliyo nayo.
kumshushia hadhi."Hayo ni maneno tu ya watu mtaani ila Mchungaji.
Gwajima ni mtumishi wa Mungu na ni uncle wangu ninawezaje kuwa na mahusiano na uncle wangu..? "Alihoji Flora.

Muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, Florah Mbasha, akichat Live leo katika ukurasa wa Facebook wa EATV.
Akijibu maswali ya mashabiki wake ambao wengi wao
wakimtaka aeleze ukweli juu ya ugomvi uliopo kati yake na Mumewe au ni
skendo tu za magazeti, ambapo aliweka wazi kuwa kuna vyombo vya habari
ambavyo vimekuwa na lengo la kumchafua na kumualibia sifa ndio maana
walitumia gharama kubwa kufanya wanavyoweza ili kutimiza malengo
yao,mbasha amedai kuwa alimua kukaa kimya kwa kuwa hakukuwa na ukweli
wowote.
"Hizo stori mnazosikia hazina ukweli wowote na
ndio maana niliamua kukaa kimya sikutaka kujibizana kwenye vyombo vya
habari kwa uongo wa baadhi ya magazeti ya
udaku ila ninasikitika sana kwani kuna watu wamekaa na kujipanga kisawa
sawa kwa ajili ya kuhakikisha wanaharibu huduma yangu kwa gharama
zozote, lakini bado ninasonga mbele kwani mwanzilishi wa huduma yangu ni
Mungu na huyo ndiye atakayeimaliza na sio mwanadamu. hata hivyo
ninawashukuru kwa kuwa wamenitabilia nkuja kumiliki jumba na magari ya
kifahari ingawa yote ni ubatili"
Adai hajaachana na Mbasha
Flora Mbasha amesema kuwa watu wengi wanasema kuwa ameachana na Mumewe
kisa Gwajima hilo swala halina ukweli wowote hajaachana na Mbasha sababu
ya Gwajima na amedai kuwa bado anampenda sana ila anampenda Mungu
zaidi.
bali amekuwa na matatizo katika ndoa yake kati
yake na mumewe na ni matatizo yao ya ndani ambayo asingependa kuyaweka
wazi katika vyombo vya habari maana kufanya hivyo ni sawa na kumvunjia
heshima mumewe,maana mambo ya chumbani ni siri yao wenyewe asingependa
kuwa wazi sababu wanamtoto mkubwa sasa.
"Sijamwacha mume wangu sababu ya Gwajima na kweli bado napenda sana Mbasha lakini nampenda zaidi Mungu"
Wakati
anazungumzia suala hili Flora ameweka wazi kuwa kwa sasa ni mjamzito na
ujauzito huo ni wa Mume wake ambaye ni Emmanuel Mbasha, maana ameishi
naye katika ndoa zaidi ya miaka kumi na katika kipindi chote hicho
hajawahi hata siku moja kumsaliti Mumewe.
0 comments:
Post a Comment