Kocha wa timu ya Taifa ya England Roy Hodgson amesema England
haijapoteza uelekeo wakati ikijiandaa na michuano ya kombe la ulaya
mwaka 2016, na kuelekea kampeni za kufuzu kushiriki michuano hiyo,
kampeni zitakazoanza mwezi ujao
Kocha wa England Roy Hodgson
England ambayo ilishindwa kufanya vizuri kwenye michuano ya kombe la
dunia katika hatua ya makundi itaanzia kampeni yake ugenini kwa
kupambana na Switzerland tarehe 8 mwezi Septemba.
Katika katika kundi iliyopangwa, England itapambana na timu za Slovenia,Estonia, Lithuania na San Marino.
Hodgson amesema ana matumaini kuwa watafanya vizuri.
England imeshuka kiwango cha ubora vya fifa
mpaka nafasi ya 20th baada ya kuchemka nchini Brazil walipopoteza mchezo
dhidi ya Italia na Uruguay, kabla ya kupata pointi dhidi ya Costarica
ambapo tayari walikuwa wametolewa
0 comments:
Post a Comment