Ethiopia na Kenya zimetangaza niya ya kutaka kuwa wenyeji wa kombe la
mataifa bingwa barani Afrika mwaka wa 2017 baada ya Libya kujiondoa
Kenya na Ethiopia zimetangaza kuwania uwenyeji wa AFCON2017
Libya ilitangaza kauli hiyo baada ya mapigano kuchacha baina ya makundi
mawili hasimu yaliyowanyima waandalizi fursa ya kujenga viwanja vipya
vya mashindano hayo.
Ethiopia, ambayo imewahi kuwa mwenyeji wa mashindano hayo katika miaka
ya 1962, 1968 na 1976, imesema kuwa itawasilisha rasmi ombi lake mara
moja
Libya ilijiondoa vita vilipochacha
Rasi wa Shirikisho la soka la Ethiopia Junedin
Basha ameiambia BYW kuwa tayari taifa hilo linaviwanja viwili
vyenye hadhi ya kimataifa (Addis Ababa na Bahir Dar), na hivyo hoja kuu
itakuwa kukamilisha viwanja viwili vipya ambavyo tayari vinaendelea
kujengwa.
"Serikali inaari ya kuyaleta mashindano hayo hapa Ethiopia ."alisema
Kenya kwa upande wake imetangaza niya ya kuandaa mashindano hayo kwa pamoja na Tanzania Uganda au Rwanda.
Shirikisho la soka barani Afrika limetangaza tarehe 30 Septemba kuwa siku ya mwisho ya mataifa kuwasilisha maombi yao.
Tangazo rasmi ya nani atakayeandaa mashindano hayo itakuwa mwakani
0 comments:
Post a Comment