Msichana anayetambulika kwa jina moja la Mary (23) anayedai kuchoshwa na kazi ya kubebeshwa madawa ya kulevya.
Msichana aliyejitambulisha kwa jina moja la Mary (23), mkazi wa Dar ambaye ni mwenyeji wa Nyegezi, Mwanza, ameangua kilio na kusema; ‘nabebeshwa madawa ya kulevya (unga), nalipwa kiduchu hadi nimechoka’.Awali, gazeti hili lilitonywa na vyanzo vyake juu ya kuwepo kwa ishu hiyo maeneo ya Manzese, Dar ambapo uchunguzi ulifanyika na kumnasa binti huyo ambaye alifunguka kila kitu.
Akizungumza na wanahabari wetu kwa uoga mkubwa, Mary alidai kwamba alichukuliwa kutoka kijijini kwao huko Nyegezi ambapo alipofikishwa Dar, alijikuta akiunganishwa kwenye mtandao wa kuuza ‘unga’.
“Nililetwa Dar mwaka jana na mwanaume mmoja, aliniahidi kunitafutia kazi, niliishi naye kama mtoto wake.“Zilipita kama wiki mbili tangu aliponileta bila kuniambia nitafanya kazi gani, siku moja ndipo akanipeleka Mitaa ya Magomeni (Dar) na kuniambia nitakuwa nafanya shughuli za kuuza unga huku nikiishi nyumbani
kwake na yeye ndiye bosi wangu.

0 comments:
Post a Comment