Libya imejiondoa kuwa mwenyeji wa mashindano ya kuwania kuwa mabingwa wa Afrika mwaka wa 2017.
Libya imekiri usalama umedorora
Ujumbe wa taifa hilo lililogubikwa na vita limesema kuwa vita
vinavyoendelea nchini humo vimewanyima fursa ya kujenga viwanja na
makao ya timu zitakazoshiriki mashindano hayo.
Kufuatia kauli hiyo shirikisho la soka barani Afrika CAF sasa
limeomba mataifa badala kutuma maombi ya kutaka kuwa wenyeji wa
mashindano hayo yanayohusisha timu 16.
Mataifa yanayotaka kuandaa mashindano hayo yana muda wa hadi septemba tarehe 30 kutuma maombi yao.
Caf itatangaza mwenyeji mpya wa mashindano hayo mwakani
Shirikisho la CAF linasema kuwa linatafuta taifa lenye uwezo wa
kuhakikishia washiriki makao usalama viwanja na muundo msingi bora wa
usafiri wao .
Mapigano baina ya makundi tofauti yamesababisha mashindano kuahirishwa.
Serikali ya Libya inakabiliwa na changamoto ya usalama baada ya
makundi ya wapiganaji yaliyopewa silaha ilikumng'oa aliyekuwa kiongozi
wa taifa hilo kwa muda mrefu Muammar Gaddafi mwaka wa 2011 kukataa
kusalimisha silaha zao.
Libya ilikuwa imeahidi kujenga viwanja 11 kwa
gharama ya dola milioni 314 za Marekani ikiwemo uwanja wenye viti
60,000 uliokuwa unastahili kujengwa katika kambi ya zamani ya jeshi
mjini Tripoli.
Miji ya Benghazi na Misrata ilikuwa
imeratibiwa kujengewa viwanja vipya lakini miji hiyo ndiyo iliyokuwa
chimbuko la vita vilivyomng'oa mamalakani Gaddafi.
Tayari ligi kuu ya Libya imeahirishwa kwa hofu ya kuwa timu shiriki zitashindwa kuhakikishia usalama wao.
Mataifa yenye uwezo wa kuandaa makala ya 2017 ya AFCON yana mwezi mmoja kutuma maombi yao
Mechi zote za kimataifa zinahusisha libya kwa sasa zinaandaliwa katika taifa jirani la Tunisia.
Sadfa ni kuwa kwa mara ya kwanza Libya ndiyo
iliyotawazwa mabingwa wa kombe la Afrika kwa wachezaji wa ligi za
nyumbani yaani CHAN .
Vilevile Caf inatarajiwa kutangaza mwenyeji wa
makala ya mwaka wa 2019 na 2021 katika mkutano wake mkuu
utakaoandaliwa mjini Addis Ababa Ethiopia 20 Septemba.
Algeria, Cameroon, Guinea, Ivory Coast na Zambia zimetangaza azimio la kuandaa mashindano hayo.
0 comments:
Post a Comment