Malori yote ya msafara wa misaada kutoka Urusi ambayo
yalisafiri bila idhini hadi katika eneo linalodhibitiwa na waasi
mashariki mwa Ukraine siku ya ijumaa yamerudi nchini Urusi.
Afisa mmoja wa forodha amesema kuwa malori kadhaa yalikaguliwa na kurudi nchini Urusi.
Zaidi ya malori mia mbili ya misaada yalisafiri
hadi katika mji wa Luhansk siku ya ijumaa,baada ya Urusi kusema kuwa
imechoka kungojea idhini kutoka kwa serikali ya Ukraine.
Urusi inasema kuwa msaada huo ulikuwa wa
kibinaadamu,lakini mataifa ya Magharibi yanasema kuwa unatumiwa na Urusi
kuvamia Ukraine.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anatarajiwa
kufanya mazungumzo mjini Kiev na rais wa Ukraine Petro Poroshenko pamoja
na waziri mkuu Arseniy Yatsenyuk.
0 comments:
Post a Comment