Video queen matata Bongo, Agness Gerald ‘Masogange’.
MAJANGA! Baada
ya kuchomoka kwenye ule msala wa awali wa madawa ya kulevya, video
queen matata Bongo, Agness Gerald ‘Masogange’ amejikuta akiteseka kwa
ishu hiyo kwa mara nyingine.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizolifikia Risasi Jumamosi, Masogange alipatwa na
msala huo mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere, Dar hivi karibuni akitokea nchini Afrika Kusini ‘Sauz’
ambapo alidakwa na polisi wa kitengo cha kudhibiti madawa ya kulevya
nchini kilicho chini ya Godfrey Nzowa.
Akisimulia
ishu hiyo, Masogange ambaye umaarufu wake mkubwa ulizaliwa katika video
ya Wimbo wa Masogange wa Abednego Damian ‘Belle 9’, alisema alikamatwa
na watu wa uhamiaji nchini baada ya kuhisiwa kuwa hati yake ya kusafiria
ina matatizo.
“Walinikamata
baada ya kuiona hati ilikuwa na ule msala wa awali lakini walinihoji na
nikawapa majibu ambayo yaliwaridhisha, wakaniachia.
Godfrey Nzowa.
“Hii
ishu inanitesa sana lakini nashukuru Mungu kwa kuwa nakamilisha
taratibu za kuwa raia wa Afrika Kusini, nitaishi kule,” alisema
Masogange alipobanwa na Risasi Jumamosi.
Juzi
wakati gazeti hili likienda mitamboni, Masogange alikuwa kwenye Ubalozi
wa Sauz nchini katika harakati za mwisho kukamilisha taratibu za kuwa
na uraia wa Afrika Kusini ambako amesema ndiko atakapokuwa akiishi.
Julai
9, mwaka jana, Masogange alikamatwa na madawa ambayo yalihisiwa kuwa ni
ya kulevya nchini Afrika Kusini, akashikiliwa na polisi kwa miezi
kadhaa.
Septemba,
mwaka jana Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg, baada uchunguzi
kukamilika na kubainika kuwa hayakuwa madawa ya kulevya bali ni kemikali
zinazotengenezea madawa ya kulevya, Masogange alitakiwa kulipa faini ya
R30,000 (Sh4.8 milioni), akawa huru.

0 comments:
Post a Comment