MSANII wa filamu aliye pia katibu msaidizi wa Bongo Movie Unity, Devotha Mbaga amepata pigo la baa yake kuteketea kabisa kwa moto.
“Ukweli imeniuma sana kwani kila kitu kimeteketea na kwa mujibu wa mashuhuda hao, moto huo umetokana na shoti ya umeme na ilitokea Jumamosi iliyopita mchana hata sielewi niseme nini maana vyote vilivyoteketea vina thamani ya milioni kumi na nane,” alisema Devotha.
Akizungumza kwa njia ya simu Devotha alisema wakati ajali hiyo inatokea hakuwepo kwani yupo nje ya Jiji la Dar ambapo alipata taarifa kutoka kwa wafanyakazi wake kwamba baa yake hiyo iliyopo maeneo ya Kigamboni iliteketea kwa moto.
“Ukweli imeniuma sana kwani kila kitu kimeteketea na kwa mujibu wa mashuhuda hao, moto huo umetokana na shoti ya umeme na ilitokea Jumamosi iliyopita mchana hata sielewi niseme nini maana vyote vilivyoteketea vina thamani ya milioni kumi na nane,” alisema Devotha.
0 comments:
Post a Comment