Sunday, August 31, 2014

Mlipuko umeharibu jengo moja la ghorofa 4 kazkazini mashariki mwa Paris na kumuua mvulana mmoja huku watu kadhaa wakiwa hawajulikani walipo 
Jengo lililolipuliwa
Watano kati ya wale waliotoweka wanadaiwa kuwa watoto.
Afisa mmoja wa huduma ya zima moto katika mji huo mkuu amesema haijulikani ni nini kilichosababisha mlipuko huo.
Msemaji huyo amesema kuwa maafisa wa matibabu wamepelekwa katika eneo hilo

0 comments:

Post a Comment