Monday, August 25, 2014

index
Na Mwandishi Wetu
PASTOR Paul Safari wa Kanisa la Dar es Salaam Pentekoste (DPC) ni mmoja wa watakaosindikiza uzinduzi wa albamu ya Uko Hapa-The Sound of Worship ya muimbaji John Lisu inayootarajia kuzinduliwa Oktoba 5 mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam chini ya udhamini wa kampuni tanzu ya muziki wa Injili hapa nchini Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Lisu, Pastor Safari anafanya vizuri katika tasnia ya muziki wa injili ambao unafikisha ujumbe la neno la Mungu kwa jamii.
Lisu alisema Pastor Safari anatamba na albamu yake ya Sifa zivume ambako pia uzinduzi huo utasindikizwa na muimbaji mwingine anayeshika kasi katika muziki wa Injili hapa nchini, George Njabiri ‘Big Man’.
Lisu alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam na mikoa mingine ya Tanzania kujitokeza kupokea uinjilishaji kutoka kwake kupitia nyimbo zilizomo kwenye albamu yake hiyo.
Alizitaja nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo ambayo imegawanyika katika maeneo mawili, ‘Part One’ ina nyimbo za Wakusifiwa, Wastahili sifa, Mataifa ya kujua, inuka, Uko Hapa, Nijaze, Nitaongozwa, Wastahili bwana, Roho Mtakatifu, Mtakatifu na umeinuliwa.
Part Two kuna nyimbo za Yu hai Jehova, Atikisa, Nijaze, Upendo, Mataifa yakujue, Umejawa na Ukuu, Fungua Macho, Haleluya na Mungu Ibariki.

0 comments:

Post a Comment