Wednesday, August 20, 2014

Rais wa Marekani Barack Obama amesema majeshi ya Iraq na yale ya Kikurd yamepiga hatua kubwa kulitwaa tena bwawa muhimu la Mosul kutoka kwa wapiganaji wa kiislamu kaskazini mwa Iraq..http://i.thestreet.com/files/tsc/v2008/photo-gallery/politics/obama-inauguration/obama-speech.jpg

 Amesema wamethibitisha kwamba wanauwezo wa kufanya kazi kwa pamoja na wataendelea kuungwa mkono na majeshi ya Marekani, ambayo tayari yamefanya mashambulio Zaidi ya anga katika eneo linalokaliwa na wapiganaji wa kiislamu
Ripoti zinasema kuwa mapambano katika juhudi za kudhibiti maeneo yanayozunguka bwawa hilo yanaendelea.

Katika hatua nyingine kundi la himaya ya kiislamu linalofanya mashambulizi dhidi ya Wakurd limekanusha kwamba wapiganaji wake wamepoteza udhibiti wa bwawa hilo.
Wakati huohuo kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis amesema jumuia ya kimataifa itakuwa na haki katika kuchukua hatua dhidi ya wanamgambo hao


0 comments:

Post a Comment