Wanafunzi wanne wa chuo kikuu cha North Carolina nchini Marekani,
wanatengeza rangi mpya ya kucha ambayo inaweza hubadili rangi katika
sehemu yoyote iliyo na madawa ya kulevya yanayotumiwa na wanaume kama
mtego kwa wasichana na wanawake kwa ujumla
Vijana hao wanasema kuwa wanawake hujipata hatarini wanapopelekwa nje au kwenye 'Date' na wanaume wenye nia mbaya nao
Wanasema rangi hii mpya ya kucha itaweza kuonyesha ikiwa kinywaji kimewekwa dawa za kulewesha kama vile GHB na Rohypno
Lengo la kampuni hio inayomilikiwa na wanafunzi hao ni kubuni teknolojia
ambazo zinawapa wanawake uwezo wa kujikinga dhidi ya ubakaji au dhuluma
za kingono
Ukarasa wao wa Facebook unasema rangi hio ya makucha inaweza kumlinda
msichana au mwanamke yeyote kwani anaweza kuingiza kidole chake katika
kinywaji alichonunuliwa na mwanamume na kuona ikiwa amewekewa chochote
humo kwani rangi hiyo ya kucha inabadili rangi ikiwa kinywaji kile kina
dawa za kulevya
Rangi hiyo inatengezwa na kampuni ya wanafunzi hao
inayoitwa....'Undercover Colours' na tayari imependwa sana na maelfu ya
watu ishara ikiwa ukurasa wa Facebook na Twitter wa vijana hao. Lakini
hisia mchanganyiko ndizo zimeshuhudiwa zaidi.
Mmoja wa wasichana walioonekana kufurahishwa na
ugunduzi huo Adam Clark Estes anayeandikia Gizmodo, alisema kwenye
ukurasa wa Facebook wa Undercover colours kwamba, ''kuna vitu vingi vya
kuchunguza ikiwa kinywaji cha mtu kimewekwa dawa yoyote ya kulewesha.
''Ila ni vigumu kubeba vifaa hivyo hasa nyakati za usiku unapokuwa
umetoka nje ya mwanamume.
Jessica Valenti anayeandikia jarida la Guardian,
alisema ''Nafurahi kuwa vijana hawa wanataka kuzuia ubakaji, lakini kwa
kuwa ujumbe huu unaelekezwa kwa wanawake kuwa wajizuie na ubakaji, sio
sawa.''
Picha hizi za wanamitindo nchini India zilizua hisia kali kwani zilileta tasiwira ya kusifu ubakaji
Jesica anasema kusisitiza kuwa waathiriwa wa
ubakaji ndio wanaopaswa kujikinga kutokana na ubakaji , ni kama
kuwalaumu waathiriwa ambao wengi ni wanawake.
''Tayari wanawake wanafanya kila juhudi kujikinga kutokana na ubakaj,'' asema Tara Culp-Ressler.
Sasa eti kukumbuka kujipaka rangi ya makucha ili
kujizuia na ubakaji kwa kuingiza kidole ndani ya kinywaji, ni jambo
linalopaswa kukemewa.''
Pia la kushangaza ni kundi moja linalopinga
ubakaji kukemea wenye kutengeza rangi hio ya makucha wakihoji je wanaume
watajipaka vipi rangi hiyo, ni vyema kukomesha ubakaji sio tu kuuzuia,
bali kuukomesha kabisa.
Kama unavyoona hapa haya ni maoni mseto kuhusu rangi hii ya makucha.
Nini maoni yako? Je unaonaje hali ya mwanamke kuweka vidole kwenye kinywaji chake ili aepuke kubakwa?
0 comments:
Post a Comment