Miliki nyumba yako leo kwa pesa taslimu au kwa mkopo wa nyumba kutoka benki washirika.
Hatua rahisi za kumiliki nyumba yako leo.
Chukua fomu ya kununua Nyumba kutoka ofisi za Shirika zilizopo kwenye mikoa yote au tembelea kwenye tovuti ya Shirika (http://bit.ly/NHChouse)
Rudisha
fomu iliyojazwa kikamilifu ikiambatanishwa na uthibitisho wa malipo ya
awali ya asilimia kumi (10%) ya thamani ya nyumba unayotarajia kununua
(ikiwa na kodi ya ongezeko la thamani yaani VAT).
Maombi
yako yatapitiwa kwa umakini ili kuhakikisha kunakuwa na usawa katika
uchaguaji wa watu wanaostahili kulingana na vigezo na masharti ya
Shirika la Nyumba la Taifa.
Wateja waliokidhi vigezo na
masharti, watapatiwa barua za uthibitisho (Letter of Offer), vile vile
wateja ambao hawajakidhi vigezo na masharti watafahamishwa kwa njia ya
barua.
Mauzo ya nyumba za mradi husika yatafungwa pindi
waombaji waliotoa malipo ya awali watafikia asimia mia moja ishirini na
tano (125%) ya idadi ya waombaji.
Mteja atapaswa
kuthibitisha mpango wa malipo wa asilimia tisini (90%) iliyobakia ya
thamani ya nyumba ndani ya kipindi cha siku 90 tangu alipopewa barua ya
uthibitisho.
Mteja anaweza kilipia nyumba yake kwa pesa taslimu, malipo ya awamu au kupitia mkopo kutoka benki washirika.
Endapo
mteja atashindwa kuthibitisha mpango wa malipo ya kumalizia manunuzi
ndani ya siku tisini, Shirika litampatia fursa mteja mwingine kati ya
waombaji walioko kwenye orodha ya maombi ya mradi husika (waiting list).
Iwapo
mteja atashindwa kukamilisha kulipia malipo ya asilimia tisini (90%)
katika kipindi kilichokubaliwa au amelipa asilimia kumi ya awali (10%)
akiwa anasubiri (waiting list) na akakosa nyumba, kiasi alichotoa
kinaweza kurudishwa au kuhamishiwa kwenye mradi mwingine iwapo mteja
atataka kufanya hivyo.
Shirika la Nyumba litafanya
utaratibu wa kutafuta hati za nyumba na kisha kuwapatia wanunuzi
waliokamilisha malipo ya ununuzi yote.
0 comments:
Post a Comment