Wanafunzi washauriwa kukaa makwao hadi Oktoba
Shule zote nchini Nigeria
zilizokuwa zianze muhula mpya jumatatu zimeagizwa kuahirisha siku ya
kufungua muhula hadi oktoba tarehe 13 kama moja wapo ya njia za
kuzuia kuenea kwa viusi vya Ebola.
Waziri wa elimu aliamuru zisifunguliwe ili kuwapa walimu mafunzo jinsi ya kushughulikia ugonjwa huo.
Watu watano wamekufa kufuatia mambukizi ya homa ya ebola nchini Nigeria .
Takwimu za maambukizi ya Ebola
Ugonjwa huu uliozuka Magharibi mwa Afrika hasa Guinea, Liberia na Sierra Leone umewauwa zaidi ya watu 1,400 .
Huu ndio uzukaji mkubwa zaidi ambapo watu 2615 wanakadiria kuambukizwa na angalau nusu yao kuaga dunia.
Virusi hivi vinaenezwa kwa wanadamu kupitia maji maji ya mwili .
Takwimu za maambukizi ya Ebola
Ugonjwa huuu hauna tiba, ila kwa kuangaliwa vyema bila shaka mtu anaweza kuishi zaidi.
Ulienea Nigeria nchi iliyo na watu wengi zaidi mwezi Julai baada ya mtu aliyekuwa na virusi kutua nchini humo kutoka Liberia.
Serikali ya Nigeria inatarajia kukomesha kuenea
zaidi kwa ugonjwa huu kwani sasa ni mtu mmoja tu aliye na ugonjwa huo
wa ebola .
Waziri wa elimu Ibrahim Shekarau amesema
Inatarajiwa angalau wafanyikazi wawili kila shule katika zile za umma na
za kibinafsi watapata mafunzo maalum ya ugonjwa huu kufikia septemba 15
jinsi ya kupambana na visa vinavyoshukiwa kuwa vya Ebola
madaktari wengi wameambukizwa Ebola.
Shirika la Afya duniani WHO lilisemakuwa mlipuko huu wa ugonjwa wa Ebola imewaambukiza madaktari wengi sana.
WHO ilitoa taarifa ambayo ilionesha kuwa zaidi
ya watu 2600 Guinea ,Liberia,Nigeria na Sierra Leone wameugua ugonjwa
huu ulioanza mei pamoja na wafanyakazi wa huduma za afya 240.
Maambukizi kwa wafanyi kazi wa afya yanatokana
na uhaba wa vifaa vya kujipinga na wafanyikazi kwani daktari mmoja
anawahudumia wagonjwa 100,000 katika nchi zingine.
WHO ilisema kuendelea kwa madaktari kuambukizwa
virusi kunapelekea juhudi za kuzuia ugonjwa huu kudidimia kwani
hospitali zingine zimeanza kufungwa.
Ebola ilivyoenea Afrika
Ebola imewauwa madaktari wa kutajika Sierra
Leone na Liberia na kupokonya nchi hizi si tu madaktari wenye uzoefu na
wanaojitolea bali waliotaka kuwa mashujaa.
Mkuu wa afya wa amarekani aliyezuru
nchizilizoambukizwa zaidi Liberia, Sierra Leone na Guinea alisema virusi
hivyo vilionekana kutawala ingawa wataalamu walikuwa na namna ya
kuukomesha.
Daktari Tom Frieden mkurugenzi wa Vituo vya
Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Marekni alisema kuwa Ingawa virusi hivi
vinaenea,Juhudi nyingi zinafanywa na kutapatikana ruzuku karibuni.
0 comments:
Post a Comment