Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini TAKUKURU imekiri kuwa rushwa bado ni changamoto kubwa kwa taifa na kutaka katiba mpya inayoendelea kujadiliwa iweke rushwa kama moja ya sura zake.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo Dr Edwad Hosea Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa taasisi hiyo uliofanyika mjini Moshi amesema nchi nyingi duniani zimeiweka rushwa kuwa adui wa uchumi na hivyo kuweka adhabu kali zinazodhibiti mianya ya rushwa.
Tanzania moja ya nchi katika Bara la afrika zinazotajwa kuwa maskini lakini zikiongoza kwa vitendo vya rushwa .rushwa amekuwa ni mdudu anayetafudiwa dawa kila kukicha pasipo mafanikio dhabiti.
Mkutano huu unaowakutanisha pamoja maafisa wasaidizi na waandamizi wa TAKUKURU kutoka nchini kote ni sehemu ya juhudi za kupata tiba dhidi ya adui huyo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akifungua mkutano huo akaelekeza maoni yake katika chaguzi mbalimbali zinazoendelea .
kwa chombo hicho,mkutano mkuu wa mwaka umearifiwa kuwa Taasisi hiyo imeokoa zaidi ya shilingi bilioni 38 kutoka sekta mbalimbali za umma zilizokuwa zimewekwa katika mazingira ya kuingizwa mifukoni na baadhi ya watumishi wa ummaa.

0 comments:
Post a Comment