Wapiganaji wa kikurdi
Jeshi la Iraq likishirikiana na
wanamgambo wa madhehebu ya ki-shia pamoja na wapiganaji wa ki-kurdi
limeanzisha mashambulizi makali ili kujaribu kuwakabilia wapiganaji wa
Islamic state ambao wameuzunguka mji wa Amerli.
Wakati huohuo idara ya ulinzi nchini Marekani
imesema kuwa ndege za kijeshi za marekani imeangusha misaa ya
kibinaadamu katika mji wa Amali uliozungukwa na islamic state.
Maelfu ya watu wamekwama katika mji
huo kwa takriban miezi miwili ijapokuwa imebainika kwamba idadi hiyo
huenda ikawa ndogo ya inavyokadiriwa.
Duru kutoka mji wa Tuz Khormutu zimeiambia BBC kwamba vikosi vya muungano vinashambulia kutoka kusini na kazkazini.
Ndege ya kijeshi ya marekani
Zimesema kuwa ndege za wanajeshi wa Iraq zinasaidia katika oparesheni hiyo na kukana kwamba ndege za marekani zinahusika.
Zimeongezea kuwa oparesheni hiyo hailengi
kuwaondoa wapiganaji hao pekee bali pia inajaribu kuifungua barabara kuu
kati ya Baghdad na kazkazini mwa taifa hilo.
Wakati huohuo wanajeshi wa Marekani wametekeleza
mashambulizi zaidi ya angani dhidi ya wapiganaji wa Islamic state
karibu na bwawa la Mosul kazkazini mwa Iraq.
Idara ya Ulinzi nchini Marekani Pentagon imesema
kuwa ndege za kijeshi pamoja na zile zisizokuwa na rubani ziliharibu
magari saba ya kivita yanayotumiwa na wapiganaji wa Islamic State.
Imesema kuwa oparesheni hiyo ni ya kuwaunga mkono wanajeshi wa Iraq na wapiganaji wa kikurdi
0 comments:
Post a Comment