Watu 5 wanaoshtumiwa kwa mauaji huko China wafikishwa mahakamani.
Watu watano waumini wa dhehebu lililopigwa marufuku nchini Uchina
wamefikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kumpiga mwanamke mmoja hadi
akafa
Watano hao wafuasi wa dhehebu la ''Church of Almighty God'' walimvamia
mama huyo katika mkahawa wa McDonalds katika mji wa Shandong ulioko
mashariki mwa China
Mama huyo Wu Shuoyan - alipigwa mbele ya mwanawe mwenye umri wa miaka 7
baada ya wafuasi wa dhehebu hilo kudai alikataa kupeana nambari yake ya
simu ya mkononi kwa mmoja wa washiriki wa dini hiyo ambaye alitaka
kumshawishi kujiunga na dini hiyo
Mauaji ya Wu yaliwatamausha wachina ambao hawakuamini kuwa watu wangeweza kutekeleza mauaji mbele ya Umma.
Duka la Mcdonalds alikouawa Wu Shuoyan
Picha za kamera za siri zilionesha mashambulizi hayo mbele ya mwanawe na
wateja wengine katika mkahawa huo ambao hawakufanya lolote kuokoa
maisha ya mama huyo
Dhehebu hilo linazaidi ya wafuasi milioni moja nchini humo licha ya kuwa limepigwa marufuku .
Mafundisho ya dhehebu hilo yanadai kuwa yesu Kristo alifufuka katika maumbili ya mwanamke wa Kichina.
Mamia ya wafuasi wa dhehebu hilo wamekamatwa nchini Uchina tangu mauaji ya Wu mwezi Mei.
0 comments:
Post a Comment