Posted by Williammalecela.com on Tuesday, September 23, 2014


 |
Kama mtakumbuka kuwa baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kutoa maneno ya uchochezi sambamba na kutangaza maandamano yasiyo na kikomo nchi nzima kwa kile alichoita kupinga fedha za walipakodi kuteketea kwenye Bunge Maalum la Katiba,
aliitwa Makao Makuu ya jeshi la Polisi nchini kuhojiwa. Aidha, wakati Mbowe akihojiwa, viongozi mbalimbali wa chama hicho ngazi ya mikoa na wilaya waliandaa maandamano ambayo hata hivyo hayakufanikiwa. Cha kushangaza zaidi, mara baada ya Mbowe kuhojiwa hapo Central Police na kuona mambo ni magumu kwake, aliamua kukimbia nchi na kwenda South Africa ambako hakuna aliyejua sababu za msingi za kwenda huko. Halikadhalika, huku Mbowe akitimkia South Africa, Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema kwa niaba ya viongozi wengine wa CHADEMA nchi nzima aliwaagiza wafuasi wa chama hicho kununua mikate ya kutosha na maji kwa vile wanaenda kwenye maandamano ambayo hayana kikomo. Pia aliwaambia wanunue mikeka ili kama wakihitaji kujipumzisha barabarani basi waitumie kama matandiko. Binafsi nimetafakari sana mambo hayo mawili yaani kuondoka kwa Mbowe na kauli ya Lema ya kuwataka wafuasi wao wanunue mikate na maji ya kutosha. Tafakari yangu imeongezwa nguvu mara baada ya mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Paul Makonda kutuwekea wazi kuwa kumbe Freeman Mbowe anagharamia malazi kiasi cha Dola za Kimarekani 700 kwa siku huko South Africa. Kiasi hicho ni kikubwa sana na nimezidi kujawa na sintofahamu zaidi baada ya kudokezwa na rafiki yangu ambaye ni kiongozi wa juu wa CHADEMA kunidokeza kuwa CHAMA ndo kinagharamia safari hiyo kwani mwenyekiti wao alisema kuwa anaenda kwa shughuli za kichama kumbe anaenda kwenye biashara zake. Nimejiuliza na nazidi kujiuliza na nadhani na wenzangu mnajiuliza na mtazidi kujiuliza, je ni sahihi kwa Mbowe kukimbia nchi na kwenda kuponda raha kiasi hicho ilhali wafuasi wake waliambiwa wanunue mikate ya kutosha na maji? Nasikia pia kuwa kudoda kwa maandamano haya kunatokana na wafuasi wao kukosa fedha za kutosha kununulia mikate. |
0 comments:
Post a Comment