Nilisema kuwa katika tasnia ya filamu, ni muigizaji mzuri kwa kupamba sinema kutokana na uzuri wa sura na umbo lake, lakini katika wasanii wanaotakiwa kwa weledi na viwango, bado ni mtu wa kati, ingawa akiwa makini zaidi katika kazi yake, anaweza kuja juu!Aunt, kama walivyo wasanii wenzake wenye majina, anavuma zaidi nje ya fani kuliko ndani. Wakati waigizaji kama Natasha, Aisha, Monalisa na Nora enzi zao walivuma kutokana na uwezo wao katika kazi wakiwa na makundi yao runingani, kizazi cha kina Aunt Ezekiel kinatikisa anga kikiwa katika kumbi za starehe na kwenye mikusanyiko ya watu!
Leo nazungumza tena na Aunt, hasa baada ya kujiuliza kwa muda mrefu na kushindwa kupata jibu, la kama muigizaji huyu yupo katika ndoa au alishaachika tena. Kumbukumbu zinaniambia aliwahi kuishi kwa kupika na kupakua na mtoto mmoja wa mjini, Jack Pemba na baadaye Hartman Mbilinyi kabla ya ndoa yake ya mwisho akiwa na Sunday Demonte.
Ingawa ni vigumu kuthibitisha, lakini ushahidi wa mazingira unaonyesha Aunt Ezekiel ni mmoja wa waigizaji wa kike ambao hawajatulia. Msanii huyu anadai yupo katika ndoa na mumewe Demonte, ambaye anaelea katika uvumi kwamba huko aliko, yupo matatizoni. SOMA ZAIDI HAPA>>
0 comments:
Post a Comment