Tuesday, September 30, 2014

Paka mwenye hirizi kubwa shingoni akiwa amepigiliwa misumari juu ya mti uliopo jirani na Msikiti wa kwa Mtawara uliopo Kata ya Mwembesongo, Morogoro.
hali isiyokuwa ya kawaida, paka mwenye hirizi kubwa shingoni akiwa hai alikutwa amepigiliwa misumari juu ya mti uliopo jirani na Msikiti wa kwa Mtawara uliopo Kata ya Mwembesongo mkoani hapa.
Tukio hilo lililokusanya umati mkubwa wakiwemo waumini wa msikiti huo lilitokea alfajiri ya Alhamisi iliyopita ambapo baadhi ya waumini wa msikiti huo walikuwa wamefika msikitini kwa Swala ya Alfajiri. 
Baadhi ya waumini wa msikiti huo walipohojiwa na mwandishi wetu walisema alfajiri hiyo walisikia sauti ya paka akilia kutoka kwenye mti huo uliopo kandokando ya Barabara ya Mtawara inayoelekea Kichangani na Mji Mpya.
Watoto wakishudia tukio hilo la kushangaza.
“Tulifika hapa msikitini kwa lengo la kuswali Swala ya Alfajiri kwa kuwa bado kulikuwa na giza hatukuweza kumwona, lakini tulisikia akilia kwa kupiga kelele mfululizo.PICHA ZAIDI>>

0 comments:

Post a Comment