Tuesday, September 23, 2014

SAKATA la mtoto Happiness (10) aliyetikisa kwa tukio la kupanda ndege kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Zanzibar bila kujulikana limeibuka tena, safari hii katika sura mpya kufuatia mtoto huyo kufungua kinywa chake na kuanika mambo ya kichawi, Uwazi lina mkanda mzima.Mtoto Happiness (10) anayeishangaza jamii kwa matukio ya kimazingara. Mtoto huyo aliyaanika mambo hayo mwishoni mwa wiki iliyopita mbele ya Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Dar, SACP Mary Nzuki na kumfanya afande huyo kupigwa butwaa. Aidha, alizungumza na Uwazi, nyumbani kwao, Mkuranga. 
ALICHOSEMA AWALI NI HIKI
Awali akizungumza kwa kujiamini, mtoto huyo ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mkokozi Kata ya Vikindu wilayani Mkuranga, Pwani, alikiri kusafiri kwa ndege hadi Zanzibar akidai alikwenda kumfuata baba yake mzazi aishiye huko. 
Hata hivyo, mama yake mzazi, Sarah Zefania alimpinga mwanaye huyo na kusema: “Baba yake haishi Zanzibar, yupo Kipunguni (Ilala jijini Dar es Salaam).”
Mtoto Happiness akiwa na mama yake KUHUSU UCHAWI
Mtoto Happiness alikwenda mbele zaidi kwa kujiongeza akisema katika maisha yake amekuwa akifanya mambo ya kishirikina lakini si peke yake. Alisema ana mshirika wake (hakumtaja jina).SOMA ZAIDI>>

0 comments:

Post a Comment