Uongozi Mpya na Baadhi ya watanzania walioudhuria
Habari zilizosambaa ni kwamba Wanajumuiya wanapinga kitendo kibaya kilichotokea kutokana na Wanajumiya watano walioleta fujo kwenye mkutano na kuhatarisha usalama wa Watanzania: Wana Jumuiya Hao wakiongozwa na Liberatus Mwangombe walikuwa ni Dotto Malongo, Salomon Chris, Salma Moshi na Ludego Muhagama. Mapendekezo kadhaa yalipendekezwa na Wanachama ikiwemo na Kuwasimimisha au kuwaonda uwanachama hawa waliohusika na kitendo hichi cha Aibu.
Pamoja na kufaili Case ya Kuishitaka Jumuiya inaonekana Liberatus Mwangome hataki kusubiri Mahakama ifuate mkondo wake.
Watu hawa watano tu(5) wanajumuiya walikuja kwenye mkutano na kufanya fujo kwa sababu zao binafsi na ililazimika kutumia vyombo vya dola (polisi) Kuwaondoa kwenye Mkutano huo. Uongozi ulisema hautovumilia kumchukulia hatua ya kisheria mtu yeyote ya yeyote atakayehatarisha usalama wa Wanajumuiya kwenye kikao chochote au shughuli zozote za jumuiya na Uongozi uliwashukuru Wanajumuiya kuonyesha moyo wa Uzalendo na kukemea tabia hii katika Jumuiya yetu.
Liberatus Mwangombe Akibishana na Bodi Memba
Polisi Wakiwafukuza Waliofanya fujo kuondoka kwenye eneo Hilo








0 comments:
Post a Comment