Kila kukicha kunaibuka vituko vingi duniani, wamo wanaosema huenda ni mwisho wa dunia! Mama mmoja almaarufu kwa jina la Mama la Mama anadaiwa kumbonda hawara wa mumewe baada ya kumwekea mtego wa fumanizi kwenye nyumba ya kulala wageni (gesti).Hawara akihaha ndani ya gesti ya White Paris (kimara) mara baada ya fumanizi. SEKESEKE
Sekeseke hilo kubwa na la aina yake lililoshuhudiwa na wanahabari wetu lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Gesti ya White Paris iliyopo eneo la Kimara-Kona jijini Dar na kusababisha umati (inzi) kujazana na kufunga mtaa.
Habari zilidai kwamba Mama la Mama alihisi mumewe anachepuka hivyo aliamua kumfuatilia nyendo zake hasa kwenye kipengele cha matumizi ya simu.Ilisemekana kwamba, Mama la Mama alichukua laini ya simu ya mumewe alipokuwa akijiandaa kwenda kazini.
0 comments:
Post a Comment