Mwanadafada ambaye ni mwanamitindo Bongo, Hamisa Mabeto akila ujana na mpenzi wake.
MAHABA niue! Mwanadafada
ambaye ni mwanamitindo Bongo, Hamisa Mabeto ameamua kumwanika mwandani
wake baada ya kumuweka kwenye mitandao ya kijamii huku akimmwagia sifa kemkem. Akipiga
stori na mwandishi wa gazeti hili baada ya kuvutiwa waya, Hamisa
alisema mwanaume huyo ni mtu ambaye anampenda sana na wana malengo ya
kuoana muda wowote kuanzia sasa na jina lake ataliweka hadharani soon! Aliendelea kusema kuwa wana miezi sita mpaka sasa na amekuwa mtu ambaye anajua nini thamani ya mapenzi kwani muda wowote akimuhitaji anakuwa karibu yake.
Hamisa Mabeto katika pozi.
“Ni
kweli ni mpenzi wangu ambaye tunapendana sana na muda wowote kuanzia
sasa tutafunga pingu za maisha kama mipango yetu ikikaa vizuri,” alisema
Hamisa.

0 comments:
Post a Comment