Jamaa mmoja anayetumia majina ya Baraka, Muba au Martha Peter amenaswa kwa kujipatia pesa kiudanganyifu akijifanya Ofisa wa Bodi ya Mikopo wa Chuo cha Ardhi kilichopo jijini Dar.Tapeli anayetumia majina ya Baraka, Muba au Martha Peter. Tukio hilo lilitokea Septemba 19 mwaka huu katika Kituo cha Afya cha Kimara baada ya tapeli huyo kumlaghai dada mmoja aitwaye Wema Raymond wakutane hapo kwa ajili ya vipimo vya ukimwi vilivyotakiwa kuambatanishwa katika fomu ya kuomba nafasi ya kazi ambayo awali dada huyo alidai kupatiwa na tapeli huyo.
Akizungumza na waandishi wetu, Wema alisema alimfahamu tapeli huyo kupitia kwa rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Rebecca, ambaye naye awali alipigiwa simu na mtu huyohuyo akimtaka kimapenzi.
Wema alisema kuwa rafiki yake alimkatalia tapeli huyo, lakini siku chache baadaye alimpigia tena akimwambia kulikuwa na nafasi ya kazi katika Chuo cha Ardhi hivyo anamhitaji yeye kwa ajili ya nafasi hiyo.
“Kwa sababu Rebecca ana kazi yake tayari aliamua kunitaarifu mimi kwa kuwa anajua natafuta kazi,” alisema Wema.Alisema alikutana na jamaa huyo ndani ya Chuo cha Ardhi na kupatiwa fomu aliyoelekezwa kujaza kisha akatakiwa kutoa shilingi 280,000 kama malipo ya fomu hiyo na gharama za mafunzo ya siku tatu ya vitendo kuhusu kazi, fedha ambazo hakuwa nazo kwa muda huo na kulazimika kumuomba rafiki yake Rebecca amsaidie.
Wema Raymond aliyetapeliwa na tapeli huyo anayefahamika kwa jina la Baraka au 'Muba'. “Baada ya kumaliza mazungumzo pale chuoni akanisindikiza hadi nje, PICHA ZAIDI>>

0 comments:
Post a Comment