Timothy
Ray Jones anakabiliwa na mashtaka kadhaa katika jimbo ambalo ndio
makazi yake la Carolina ya kusini,kufuatia shutuma hizo na alikamatwa
mwishoni mwa wiki iliyopita huko Mississippi .
Watoto
hao watano waliopoteza uhai kwa kuuawa na baba yao walikuwa na umri wa
kuanzia mwaka mmoja hadi miaka nane ambapo inaelezwa watoto hao
walipotea katika mazingira ya kutatanisha jambo lililomfanya mama wa
watoto hao aripoti polisi baada ya mawasiliano kati yake na mzazi
mwenziwe kukatika.
Maafisa
hao wa polisi walipofanya uchunguzi wao waligundua kuwa miili ya watoto
hao ilikuwa imezikwa karibu na mji wa Alabama jirani na barabara kuu
baada ya kuwasaka watoto hao kwa siku nzima .
Jones
alisimamishwa katika kizuizi cha barabarani na kushukiwa kuwa alikuwa
akiendesha gari baada ya kutumia dawa za kulevya ambapo imethibitika
kuwa katika gari yake kulikuwa na kemikali zinazoaminika kua dawa za
kulevya na zaidi ya hapo polisi walikuta damu garini mwake na alikuwa
akitafutwa huko Carolina ya kusini.
Kitengo
kinachoshulikia usalama wa raia huko Alabama kimesema kupitia kwa
msemaji wake sajenti Steve Jarrett kwamba baada ya msako huo Jones baba
wa watoto hao aliwaongoza maafisa hao hadi eneo alikozika miili ya
wanawe.
BBC
BBC
0 comments:
Post a Comment