Makabiliano nchini Iraq
Marekani imetekeleza mashambulizi ya angani dhidi ya wapiganaji wa Islamic State karibu na bwawa la Hadatha magharibi mwa Iraq.
Ni mara ya kwanza kwa wanajeshi wa Marekani
kuendeleza mashambulizi yao ya angani hadi katika mkoa wa madhehebu ya
kisunni wa Anbar.
Maafisa wa Marekani wamesema kuwa mashambulizi
hayo manne ni ya kuwaunga mkono wanajeshi wa Iraq ambao wanalidhibiti
bwawa la hadatha lililopo mto Euphrates.
Waziri wa ulinzi nchini humo Chuck Hagel amekana
madai kwamba mashambulizi hayo ni ongezeko la ushirika wa Marekani
nchini Iraq,akisema kuwa bwawa la Hadatha ni kiungo muhimu cha Iraq na
kwamba maslahi ya Marekani yatatishiwa iwapo bwawa hilo litatekwa
0 comments:
Post a Comment