Mshauri wa Mkurugenzi Mtendaji wa Geita Gold Mine katika masuala ya serikali na jamii Bw. Clement Msalangi (mbele kwa mbali) akielezea mafanikio ya mgodi wa Geita Gold Mine katika utoaji wa huduma bora kwa jamii na uwezeshaji kwa timu ya majaji na sektretarieti iliyofanya ziara katika mgodi huo.
Meneja Mahusiano ya Jamii Bw. Manase Ndoloma akisisitiza jambo katika kikao kilichoshirikisha uongozi wa mgodi wa Geita Gold Mine na jopo la majaji na sekretarieti kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji iliyotembelea mgodi huo.
Mtaalamu katika masuala ya mahusiano na maendeleo ya jamii Bw. Joseph Mangilima ( wa pili kutoka kulia) akielezea mchango wa mgodi wa Geita Gold Mine katika mradi wa maji mbele ya bwawa la Nyankanga ambalo maji yake yatasafishwa na kusambazwa kwa wananchi wa Geita kupitia ufadhili wa mgodi huo.
Meneja Mahusiano ya Jamii Bw. Manase Ndoloma (katikati) akielezea majaji na sekretarieti mchango wa mgodi wa Geita Gold Mine katika ujenzi wa nyumba mpya kwa ajili ya wakazi wa Geita waliohamishwa kwa ajili ya kupisha shughuli za mgodi huo.
Mtaalamu katika masuala ya mahusiano na maendeleo ya jamii Bw. Joseph Mangilima ( wa nne kutoka kushoto mstari wa mbele) akiongoza timu ya majaji, sekretarieti na wataalamu wengine kutoka mgodi huo katika ziara kwenye kituo cha watoto yatima cha Moyo wa Huruma, kinachofadhiliwa na mgodi huo.
0 comments:
Post a Comment