MUUNGANO wa Wahariri umewaandikia makarani wa Bunge la Kitaifa na Seneti kulalamikia mswada wa kuongeza bunge mamlaka ya kudhibiti jinsi shughuli zake zitakavyoripotiwa.
Bw Adan Keynan. Picha/MAKTABA
Wahariri hao wakiongozwa na mweyekiti wao Linus Kaikai, wametishia kuelekea mahakamani iwapo wabunge hawatabadilisha vipengele tata vya mswada huo kabla ya kuuidhinisha.
Wahariri hao wakiongozwa na mweyekiti wao Linus Kaikai, wametishia kuelekea mahakamani iwapo wabunge hawatabadilisha vipengele tata vya mswada huo kabla ya kuuidhinisha.
“Tunasikitika kuwa kwa muda wa miezi 15 iliyopita vyombo vya habari vimeshuhudia juhudi za kukandamizwa na viongozi ambao wanalenga kuficha vitendo vyao. Mswada huu unawanyima wanahabari nafasi ya kuwafahamisha wananchi shughuli za bunge. Huu ni ukiukaji wa katiba inayotoa uhuru wa wananchi kutoa na kupokea habari,” alisema Bw Kaikai.
Bw Kaikai alipuuza madai kuwa mswada huo unalenga kulinda nguvu na mamlaka ya bunge ili litekeleze majukumu yake bila kuingiliwa na idara nyingine.
“Wabunge kama wawakilishi wa wananchi wana jukumu la kufahamisha umma shughuli zao. Mswada huu unalenga kunufaisha watu fulani ambao wanaogopa utendakazi wao upigwe msasa na Wakenya,” akaongeza.
Mswada huo ambao ulidhaminiwa na mbunge wa Eldas Bw Adan Keynan unapendekeza waandishi wa habari kupigwa faini ya Sh laki tano ama kupewa kifungo cha miaka 2 iwapo wataripoti kwa njia itakayoonekana 'kuhujumu’ bunge.
0 comments:
Post a Comment