Thursday, September 25, 2014

Khadija Kopa ameanza kuyasimulia maisha yake, amekwenda kuanza shule hukumoyo wake ukiwa na hofu kwa kuona kwamba sasa ni wakati wa kuchapwa fimbo kama walivyokuwa wengine.
Malkia wa mipasho tanzania, Khadija KopaAnaishi na bibi yake, bi Biubwa lakini mara kwa mara mama yake amekuwa akifika hapo kwa ajili ya kumsalimia.
Maisha ya bibi yake yakaanza kumfanya kudeka sana kwani hakuwa akichapwa wala kufokewa kitu kilichoonekana kuleta usumbufu hapo baadaye.
Siku hiyo nikaoneshwa darasa ambalo nilitakiwa kuwepo na kuanza masomo rasmi. Hakukuwa na mwanafunzi aliyekuwa akisoma, kwa sababu tulikuwa wadogo, muda mwingi tulikuwa tukipiga stori tu na vurugu za hapa na pale.
Katika kusoma kwangu shuleni hapo, nikabahatika kupata marafiki wengi, ila asilimia kubwa walikuwa wanaume. Ninaowakumbuka, mmoja alikuwa Salum na mwingine aliitwa Mohammed.

Hao ndiyo nilikuwa karibu nao, nilicheza nao na kula wote shuleni. Nilipokuwa sina hela, walichokuwa wakinunua tulikula wote kitu kilichonifanya kuwa karibu nao kwa kiasi kikubwa.
Alikuwa akiwaachia madaftari marafiki zake

Kwa sababu nilipenda sana michezo shuleni, kuna siku nyingine tulipotakiwa kurudi nyumbani, niliwakabidhi madaftari yangu wenzangu wanipelekee nyumbani na mimi kubaki shuleni nikicheza.

Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu, japokuwa nilitakiwa kusoma lakini wakati mwingine michezo ilionekana kuwa bora zaidi ya masomo. Kila nilipokuwa nikirudi nyumbani, bibi alikuwa akiniambia kwa upole kwamba sikutakiwa kuwakabidhi watu madaftari yangu bali nilitakiwa kurudi nayo nyumbani mwenyewe. 

BIBI AMDEKEZA
Bibi alinidekeza kama yai, hata pale nilipokuwa nikifanya makosa ambayo nilitakiwa kufokewa au kuchapwa, alikuwa akiniambia kwa sauti ya upole mno. Maisha niliyokuwa nikiishi naye, alionekana kwamba alitaka kunifundisha mengi kuhusu maisha.
Nilifurahi japokuwa na mimi nikaongeza ujeuri zaidi. Hata yale mambo mabaya, kwangu niliyaona mazuri na kuyafanya, bibi akabaki akiniambia maneno ya upole tu, alikuwa akinipenda mno na hakutaka kunikasirisha Khadija mimi.
** 
Japokuwa nilikuwa mtoto mdogo lakini niliutambua upendo ambao mama yangu alikuwa akinionesha. Alikuwa mama wa kipekee sana ambaye kila siku ilikuwa ni lazima afike nyumbani hapo na kunijulia hali.
Nilikuwa nikiishi na bibi lakini kama inavyojulikana kwamba damu nzito kuliko maji, nilipokuwa na mama nilijisikia furaha zaidi.

0 comments:

Post a Comment