Stori: Makongoro Oging’
DA! Duniani kuna mambo jamani! Katika hali isiyo ya kawaida, maeneo ya Tandale Kwatumbo jijini Dar, waombolezaji hawakuamini macho yao wakati walipomuona ‘marehemu’ Mohamed Salum ‘Fido’ (29) (pichani), akirejea nyumbani hapo huku maandalizi ya mazishi yake yakipamba moto na waombolezaji, hasa mkewe, mtoto na ndugu wakilia kwa uchungu kufuatia ‘kifo’ chake.Kijana Mohamed Salum ‘Fido’ anayesadikiwa kuwa alikufa.
Tukio hilo la aina yake lilitokea Septemba 12, mwaka huu, saa sita mchana wakati shughuli mbalimbali za mazishi yake zikiendelea zikiwa ni pamoja na maandalizi ya chakula cha mchana kwa waombolezaji.Iko hivi; Fido ni dereva wa bodaboda, kijiwe chake kikiwa Lumumba Mnazi Mmoja, Dar. Inadaiwa kwamba Septemba 10, mwaka huu alikamatwa na polisi wa ‘Tigo’, Lumumba kwa madai ya kutokuwa na kibali cha kuingia mjini, akapelekwa Kituo Kikuu cha Polisi (Central).
Pale kituoni, habari zinadai maafande hawakumruhusu kumpigia simu mkewe ili kumweleza yaliyompata, ndipo ndugu walipoamua kumtafuta kwa siku mbili bila mafanikio.
0 comments:
Post a Comment