Malkia wa muziki wa R&B, Lady Jay Dee amedai kuwa maadui zake wamebuni njia mpya ya kumwangusha, baada ya zile za awali kutofanikiwa.
Katika waraka mrefu aliouandika katika mtandao wa facebook, Lady Jay Dee alisema watu wasiopenda mafanikio yake wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali kumwangusha, lakini hata hivyo wameshindwa.
Jay Dee analalamikia habari iliyoandikwa juu yake kuwa amekuwa katika uhusiano mpya na kijana aliyemzidi umri, jambo analosema halina ukweli.
Habari hiyo inahusishwa na kile kilichodaiwa kuwa mwanamuziki huyo ameachana na mume wake, Gadner G Habash, ambaye ni mtangazaji wa kituo cha redio Times FM.
Jide ameandika: “Hata kama nimeachana na mume wangu, siyo sababu ya kunihusisha katika uhusiano na mwanamume mwingine yeyote. Habari hii imenivunjia heshima. Nafikiri lengo la uzushi huu ni kumfanya Lady Jaydee aonekane mtu asiyefaa.”
Habari hiyo ilipambwa na picha ambazo alizipiga mwenyewe kwa kutumia simu ya mume wake.

0 comments:
Post a Comment