Mohamed Abdallah Kiumbe,'Chif kiumbe' mwenye kanzu yanjano.JINA alilopewa na wazazi wake ni Mohamed Abdallah Kiumbe, lakini baada ya mihangaiko yake huku na kule, akipiga hatua taratibu za maendeleo, akajikuta amepata umaarufu mkubwa mno, sasa akijulikana kama Chief Kiumbe.
Ninamfahamu kiasi huyu jamaa, ni mchangamfu, mtu wa watu, lakini usisahau, ni kijana wa kisasa. Enzi hizo ukikutana naye kwenye kumbi za starehe, huwezi kumtofautisha na wasanii wa kileo kwa mavazi yao, pamba kali, mikufu ya dhahabu shingoni na mikononi na utitiri wa wapambe.
Kila anayepita kwenye anga zake lazima anukie ua waridi. Amewasaidia watu wengi sana, hasa wasanii wa muziki wa dansi na Bongo Fleva. Amewasimamia baadhi ya watu wenye majina makubwa kama Profesa Jay, Q Chilla, Hussein Machozi, Matonya na wengine wengi.
Kwa taarifa ya ziada, ndiye mhimili mkubwa wa mafanikio ya Extra Bongo. Kama kuna watu ambao Ally Choki hawezi kuwasahau anapoizungumzia bendi yake, basi ni huyu jamaa.
0 comments:
Post a Comment