Nyota wa filamu Bongo, Lucy Francis Komba na mzungu wake raia wa Denmark anayejulikana kwa jina moja la Janus wakiwa ni wenye furaha wakati wa harusi yao.
ILE NDOA ILIYOKUWA IKISUBIRIWA KWA MUDA MREFU YA NYOTA WA FILAMU BONGO, LUCY FRANCIS KOMBA NA MZUNGU WAKE RAIA WA DENMARK ANAYEJULIKANA KWA JINA MOJA LA JANUS HATIMAYE IMEFUNGWA NA KUTAWALIWA NA MATUKIO YENYE MIKOSI KIBAO.
Ndoa hiyo ilifungwa Jumamosi iliyopita kwenye Kanisa la Roman Katoliki Parokia ya Mtakatifu Benedict lililopo maeneo ya Kurasini- Bandari jijini Dar.
Baada ya zoezi hilo kumalizika, wawili hao na wapambe wao walikwenda katika Kisiwa cha Bongoyo, Dar kwa ajili kupiga picha za ukumbusho. Kisiwa hicho kipo Kilomita 2.5 kutoka Pwani ya Jiji la Dar.
Hata hivyo, zoezi la kwenda kupiga picha kwenye kisiwa hicho liliingia mkosi kufuatia maharusi hao kupanda boti maeneo ya Slip Way, Oysterbay, Dar na kupigwa na mawimbi makubwa yaliyowafanya watumbukie baharini kabla ya kuokolewa na wapiga mbizi mahiri.
0 comments:
Post a Comment