
Charles Gabriel ‘Chaz Baba’.KWAKO jembe, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’. Mwalimu wao kwenye muziki wa dansi Bongo. Uwezo wako nautambua, nimekuwa shabiki wako kwa muda mrefu kidogo.Ni matumaini yangu uko poa, unaendelea na mishe zako kama kawaida.
Mimi mzima, namshukuru Mungu maisha yanasonga. Jukumu langu la kuandika na kukosoa linaendelea na leo nimekukumbuka wewe.Dhumuni la kukumbuka leo kwanza ni kukukemea kwamba suala la kuthubutu kushika kitu kizito, kunyanyua mkono na kumtwanga mtu si jambo jema, halifai kuigwa hata kidogo.Ndugu yangu, hivi kwanza unafikiria nini ukichukua kitu kizito na kumpiga nacho mwenzako?Mbona zipo njia nyingi za kufikisha ujumbe wako kwa mtu na akajua umekasirika, lakini si kumtwanga na kitu kizito au chenye ncha kali ambacho unajua fika kwamba utamsababishia maumivu makali mwilini.
Kwa kitendo ulichokifanya kwa mkeo hivi karibuni hakikuwa cha kiungwana. Ulimtwanga kiasi ambacho kwa macho ya kawaida tu, inaonesha aliumia sana.Sitaki kujua alikuudhi nini, lakini ustahimilivu unatakiwa katika maisha ya kila siku.
Hata iweje yule ni mkeo. Unajisikiaje kumuona akiwa na majeraha chungu nzima mwilini ambayo umesababisha wewe? Si sawa kabisa!Wewe ni kioo cha jamii, unategemea jamii itajifunza nini kupitia tukio kama lile ulilolifanya? Unavyotakiwa kujichunga wewe ni mara mia zaidi ya vile anavyojichunga mwenzangu na mimi kule Tandale Kwa Mtogole. SOMA ZAIDI>>
0 comments:
Post a Comment