Mashambulizi nchini Ukraine
Milipuko mikali imesikika katika mji wa Bandari wa Mariupol mashariki mwa Ukraine.
Waandishi walioshuhudia makombora hayo wanasema
kuwa kizuizi muhimu cha serikali kiliharibiwa na mashambulizi makali
kutoka kwa wapiganaji wanaounga mkono Urusi.
Mashambulizi makali ya kulipiza kisasi pia yamesikika.
Mji wa Mariupol unaonekana na wapiganaji
wanaounga mkono Urusi kama muhimu katika barabara inayoelekea Crimea
mbali na kuwa kitega uchumi cha eneo la Donbas iwapo litakuwa huru.
Mwandishi wa BBC katika mji huo amesema kuwa
haijulikani iwapo mashambulizi hayo ni ya mda ama ni mwisho wa
makubaliano ya kusitisha vita yalioafikiwa siku ya ijumaa.
Awali viongozi wa Urusi na Ukraine walisema kuwa wameridhika kuwa makubaliano hayo yanaafikiwa.
Rais Vladmir Putin na mwenzake wa Ukraine Petro Porishenko walizungumza kuhusu mwafaka huo kupitia njia ya simu.
Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu
limesema kuwa makombora yaliyalazimu malori ya misaada yaliokuwa
yakielekea katika mji unaodhibitiwa na waasi wa Luhansk kurudi
0 comments:
Post a Comment