BAADA ya hivi karibuni siri kufichuka kwamba Kundi la Bongo Movie linateswa na laana ya marehemu Steven Kanumba, mama yake Flora Mtegoa ameibuka na kueleza mazito yakiwemo ya aliyekuwa rafiki wa mwanaye, Vincent Kigos ‘Ray’,mchapo kamili huu hapa .
Mama yake marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa. Akizungumza kwa hisia kali Mama Kanumba alisema anaungana na katibu msaidizi wa klabu hiyo, Devotha Mbaga kwamba kundi hilo lina laana ya Kanumba kwani naye kama mzazi ni shahidi kutokana na mwanaye kila wakati alikuwa akimfuata nyumbani akilia na kusema kwamba hawatakaa waelewane milele.
“Kanumba alikufa akiwa ameshajitoa Bongo Movie kutokana na majungu waliyokuwa wakimwandama kila kukicha na maneno yake ya siku chache kabla hajaaga dunia alikuwa akisema kwamba kundi hilo halitakaa lielewane milele kwa kuwa walikuwa wakimchukia na kumsemea majungu bila sababu hali iliyokuwa ikimsababisha kulia na kulalama kila wakati.
Aliyekuwa rafiki wa Kanumba, Vincent Kigos ‘Ray’. “Alisema ukweli ni kwamba kundi hilo linakosa kuwa na maendeleo kwa sababu wanaendekeza majungu hivyo akaniambia mama nimejitoa huko japokuwa mimi ni mmoja wa waanzilishi yaani sitaki tena,” alisema Mama Kanumba.
0 comments:
Post a Comment