Manchester United imeripoti kupata hasara kubwa ya kipato chake cha kila
mwaka licha ya kuonesha faida nzuri wakati wa uongozi wa David Moyes
kama maneja
Klabu hiyo ya Uingereza, inasema kuwa kipato chake cha kila mwaka
kilishuka kwa asilimia 84, ilihali faida yake iliongezeka kwa zaidi ya
asilimia ishirini.
Inasema kuwa inatarajia kipato chake cha mwaka
2015 kushuka, kutokana na kuzidi kuandikisha matokeo mabaya, hasa katika
mashindano ya ligi kuu kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20.
Aidha,
matokeo hayo pia yanaonesha kuwa Moyes na wafanyakazi wake walipata
jumla ya Dola milioni nane kama malipo ya kuachishwa kazi mapema mwaka
huu baada ya kuwa ofisini kwa chini ya mwaka mmoja
0 comments:
Post a Comment