Matangazo ya tiba za asili yanaelezwa kupotosha umma
Baraza la Tiba za Asili na Tiba Mbadala Tanzania
limesitisha vibali vya kurusha matangazo ya tiba za asili na mbadala
kwenye vyombo vyote vya habari kwa kile kilichoelezwa kuwa yanapotosha
jamii.
Taarifa iliyotolewa na kwa vyombo vya habari ,
imeeleza kuwa katika siku za karibuni kumekuwapo na matangazo mbalimbali
ya tiba hizo ambayo baadhi yake hayaisaidii jamii.
Kutokana na taarifa hiyo ya baraza, vyombo vya
habari havipaswi kupokea kibali chochote cha kutangaza matangazo ya tiba
hizo hivi sasa, kwa kuwa ni batili.
Pia taarifa hiyo inaeleza kuwa, chombo chochote
kitakachorusha tangazo au kipindi kitatozwa faini na kuchukuliwa hatua
kali za kisheria.
naye mtaalam wa tiba asili, tabibu Rahabu Rubago
ameiambia BBC kuwa hatua hiyo ya Baraza imetolewa bila wao kupatiwa
taarifa hiyo mapema na kueleza kuwa watapata hasara kwa kuwa baadhi yao
wametengeneza vipindi tayari kwa ajili ya kuvirusha kwenye vyombo vya
habari
0 comments:
Post a Comment