Rais Jakaya Kikwete
Kumekuwa na maoni tofauti kufuatia hatua ya kusitisha mchakato wa kura ya maoni ya Katiba Mpya nchini Tanzania.
Katika
kikao cha Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na Viongozi wa vyama vya
siasa nchini humo wamekubaliana kuwa kura hiyo ya maoni ambayo ilikuwa
ifanyike kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 kinafanyika baada ya uchaguzi
huo
Umoja wa wabunge wa kambi ya upinzani Tanzania UKAWA hivi
karibuni walisusia bunge la Katiba na kutoka nje kwa kile walichodai
kutekelezwa kwa baadhi ya madai ya msingi.
Akizungumza na BBC
Deusi Kibamba Mwenyekiti wa jukwaa la Katiba nchini Tanzania anasema
hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa kusitisha vikao vya bunge la
katiba hata kabla ya muda uliopendekezwa wa Oktobar 4 mwaka huu.
Amesema
kuwa iwapo wabunge hao wataendelea na vikao hivyo wao pamoja na baadhi
ya wananchi wanatarajia kufanya maandamano hadi mjini Dodoma na kufunga
milango ya ukumbi wa bunge.
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na
kijamii Robert Mkosamali anasema pamoja na kwamba fedha nyingi
zimekwisha tumika hadi sasa kinachpaswa kuangaliwa si gharama hizo bali
ni kuangalia ubora wa katiba inayotafutwa hata kama yaweza kutafutwa kwa
muda mrefu na wka gharama kubwa.
Mkosamali amesema hata nchi zilizopata Katiba zilichukua muda mrefu na gharama kubwa akitolea mfano nchi ya Kenya
0 comments:
Post a Comment