Wednesday, September 24, 2014

Nuru Ramadhani Nasibu, mkazi wa jijini Dar es Salaam anayetuhumiwa kwa wizi wa magari.
Nuru Ramadhani Nasibu (pichani), mkazi wa jijini Dar es Salaam aliyekuwa akitafutwa na polisi wa nchini na wa kimataifa (Interpol) kwa kuhusishwa na wizi wa kuaminiwa wa magari matatu mali ya Dk. Emmanuel Matech  ametiwa mbaroni.Taarifa zilizopatikana ndani ya jeshi hilo juzi zinadai mwanamke huyo alitiwa mbaroni hivi karibuni na kwa sasa jalada la kesi yake linaandaliwa kwenda kwa mkurugenzi wa mashitaka nchini (DPP) kwa hiyo yupo nje kwa dhamana.
Kabla ya kutiwa mbaroni kwa mwanamke huyo ambaye ni mke wa kigogo wa ulinzi wa kampuni ya taasisi moja ya umma nchini, Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kwa kupitia ofisi ya mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai liliandika barua Julai 13, mwaka huu iliyokuwa na namba ya jalada OB/IR/5705//2014 wizi wa kuaminiwa.
Katika barua hiyo, magari matatu yalitajwa kuibwa kwa kuaminiwa na mwanamke huyo ambayo ni Toyota Harrier (namba T 948 CGV), Toyota Prado (T 928 CJS) na Toyota Rav 4 (T 673 BXR) na mtuhumiwa ametajwa kwamba ni Nuru ambaye alikuwa bado hajakamatwa.SOMA ZAIDI>>

0 comments:

Post a Comment